Tuesday, October 14, 2014

HII NI KWA WANAWAKE NA WASICHANA WANAOPITIA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZA KIMAISHA.


umekuwepo na hali ya kuchaguliana nini cha kufanya kwenye maisha.Hali ambayo hupelekea wengine kupata msongo wa mawazo kisa kuona hawakubaliki katika jamii fulani.Au kuona kuwa hathaminiki kisa ana utaratibu flani wa kimaisha tofauti na wengine.
Kumcheka mtu kwa sababu ya muonekano fulani bila kujali kuwa huo muonekano umekuja baada ya kupitia changamoto fulani katika maisha.Wakati mwingine wanawake ndio hao hao hukaa na kunyoosha vidole kumcheka mwanamke mwenzao.Wasichana wanamkejeli na kumdhihaki msichana mwenzao kisa muonekao or style flani ya maisha.Nimetumia mfano wa wanawake kwa sababu ndio wanaongoza kwa tabia hiyo dhidi ya wanawake wenzao.

Picha hizi ni kazi ya mwanadada Carol Rosseti wa Brazil.Amechora na kutengeneza picha hizi kuwatia moyo na kuiasa jamii kuacha maneno ya dharau na kejeli kwa wanawake.
 


b







Je wewe upo wapi?

4 comments:

  1. Dina umenigusa sana na kichwa cha habari, ni kweli kabisa wanawake tuna tabia hiyo sana ya kusema watu, nimeolewa miaka 6 bila mtoto nimeenda hospital vipimo vyote nimemaliza naambiwa niko ok, mume wangu ka mpa mimba mwanamke mwingine, nime gundua post FB huyo dada alikua ananitukana kama vile niliomba kutokuzaa nimeumia sana na shukuru sala zimenipa ujasiri, kikubwa wa kina mama , dada na wasichana tuacheni tabia za kumsimanga mtu kwa jinsi alivyo, umbile au sura hakupenda kuwa hivyo alivyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. polee sana my dear i can imagine unajisikiaje.Ila utashinda tu na utapita mtihani huo.

      Delete
  2. Pole dear I can feel jinsi unavyojisikia but nikutie moyo kwamba one day yessss na ww utanyonyesha mtoto wako na nmefurahi pia kwa vile unamwamini Mungu huyo anaekutukana mwache aendelee kaa kimya maana nalo ni jibu pia Mungu ndio atamuhukumu....

    ReplyDelete
  3. Binafsi sipendi kushave kama huyo Amanda, I know ni usafi sijui unavutia...lakini mi ndo sipendi hivo, ntajiosha na kujisafisha vizuri lakini kushave huwa nanuna kabisa kama nimelazimishwa. Sababu kubwa inayonifanya niwe hivi ni speed kubwa ya ukuwaji wa nywele hiz, yaani nikishave nakaa wiki na kidogo zishastawi....i hate!

    ReplyDelete