Tuesday, October 21, 2014

NI WAJIBU WAKO KAMA MZAZI KUMJENGEA MTOTO WAKO KUJIAMINI.

Huwa nasoma sana website inaitwa woman of christ nilikutana na huu ujumbe nikapenda kushare nanyi.Hasa wazazi itawafaa katika malezi.

Mzazi ni wajibu wako kuwapenda watoto wako wote, kuwafundisha njia ipasayo, kuwatia moyo wanapopitia magumu, na kuhakikisha unakuwa mstari wa mbele kuwajengea self esteem imara. Mzazi hupaswi kuwa critic wa mtoto wako, hiyo sio kazi yako. Muongoze katika kweli, mfundishe, muadhibu pale anapokosea na chunga sana usimuadhibu ili kumuaibisha bali kumsaidia. Adhabu ya kumsaidia mtoto unampa kwa kujali utu wake na sio mbele ya kadamnasi na kumuaibisha.
Watoto hawalingani, usifanye kosa la kuwalinganisha watoto, iwe ni watoto wako wote au kumlinganisha wako na wa jirani. Tambua kila mwanadamu ameumbwa tofauti, jitahidi kumfahamu mwanao na kumsaidia kuwa bora kwa jinsi Mungu alivyomuumba ukiangalia zaidi strengths zake kuliko mapungufu. Kosa ambalo wazazi wengi wanafanya ni kuwabagua watoto kulingana na uwezo wao kwa yale ambayo yanaonekana mema katika jamii mfano kumpenda zaidi mtoto anayejituma kuwahi kuamka na kumbeza yule anayependa kulala tena mbele za wengine. Ndio, kila mtoto lazima afuate utaratibu lakini usitumie kigezo hiki kupimia upendo, badala ya kumsaidia utakuwa unampoteza kabisa.

Mtoto anayeona anabaguliwa nyumbani atajenga kiburi na ataanza kuwachukia wenzie wanaopendwa zaidi na itampelekea kutafuta upendo nje kwa watu wasiofaa na kujikuta katika matatizo makubwa. Chunga sana maneno unayomwambia mtoto wako, maneno yanaumiza kwa muda mrefu, yanaua kujiamini na yanaumba. Mtamkie maneno ya baraka, tumaini na hata pale unapomuonya maneno yako yasiwe ya kumdhalilisha mfano hujui kitu kabisa, sijui wewe ni mtoto wa aina gani, hufai kabisa n.k. Maneno ya aina hiyo hayafai kabisa maana hayajengi bali yanamuondolea kujiamini na kumfanya ajione hana thamani.

17 comments:

  1. Agreed dina. Mama yangu ni mtu maisha yangu yote anatumia maneno ya kumshusha mtu. Hadi anafika kusema why did i have kids..au unafkiri wewe mzuri nani atakupenda? Yaliniumiza sana lakini nashkuru Mungu kanipa roho ya msamaha sikuyatilia sana maanani na ninampenda sana mama yangu. Lakini Imenijenga and i vowed never to use such language with my children maana i know how painful it is bora ucharazwe viboko ukikosa.

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa,unajua wazazi wengi hawawezi kuzuia hasira zao inawapelekea kuwaambia maneno yasiofaa, mi nilikutana na tatizo kama hilo yaan ilipelekea kumchukia mama yangu tangu nikiwa darasa la tatu mbaka miaka mitatu iliyopita ndo nimerudi sawa yaan nilikuwa nakutana na changamoto nyingi ila sikuwa na wakumwambia mama yangu alikuwa bizy na ndugu zangu watatu ila namshukuru Mungu nimeolewa nw na mume wng amenisaidia sana kuondokana na tatizo mbaka sasa hivi nampenda Mama yangu na namuombea kwa Mungu maisha marefu.Wazazi tuangalie kauli zetu mana madhara yake huwa ni makubwa sana

    ReplyDelete
  3. Dada dina naomba email yako tafadhali

    ReplyDelete
  4. Hello Dina, naomba email yako please.

    ReplyDelete
  5. Hello Dina, naomba email yako please.

    ReplyDelete
  6. Dina Hii imenigusa sana kama mzazi kwasasa lakini pia imenirudisha nyuma kiasi ktk maisha yangu binafsi, Ishort nimelelewa na mama wa kambo nikapitia magumu ambayo nilihisi upweke uliopitiliza. Akatokea mtu kunionyesha ninathamani, nastahili kupendwa na kujaliwa. Nilijikuta naingia ktk mapenzi when I was only 15yrs. Nashukuru niliyekuwa nae alikuwa amepevuka zaidi kiakili hivyo haikunipa matatizo yoyote hasi. Tulitengana baada ya three years ila ninamshukuru alinisaidia kujitambua mapema. Niliweza kusongambele hata baada ya mama yangu mzazi kufariki (which meant lonelyness as the name itself) but he was there for me. Namuombea Mungu ambariki popote alipo. Wazazi tuzidi kujifunza na kuwajibika ipasavyo juu ya nafasi zetu ktk familia.

    ReplyDelete
  7. dada dina me nilianza kuishi na mamkubwa tangu I was5or6.. 5 mama hakuwa ananijali ndo maana akanichukua mamkubwa...now am26 ckuwahi tena kuishi na mama angu..hd leo hii..mamkubwa akafa nina miaka10..nikaenda kuishi na shangqzi.... Baada ya hapo nikaenda kuishi na baba angu na mama wa kambo..sio siri sioni raha ya mama hapa ukiniuliza...mama kaanzackunitafuta nimeanza kazi... Nimtumie hela za matumizi...nicpotuma ananuna...anawajali wadogo zangu tulioshera mama tu..me ndo wa kwanza lkni naona kabisa mapenzi yake niliyakosa..hv juzi nimepamta mchumba wa kiislam mama kajitoa hataki kujihusisha na chochote

    ReplyDelete
  8. ni kweli kabisa kisaikologia mtoto anayebaguliwa hata km ni mtundu kiasi atakua hajiamini wapendwa ninauza products za foreva living karibuni maswala ya claen 9 moyo kisukari watoto wasiopenda kula wanaougua mr kw mr nitafute namba yng ni 0769119295 nimeweka namba maana najua humu ni wastaarabu

    ReplyDelete
  9. mimi ninatatizo tu jamani naomba ushauri hivi unaweza ukawa umeweza kubeba mimba zaidi ya mara tatu na mirija ikaziba? je unaweza ukakosa kushika mimba ? nombeni mwenye uzoefu anijibu.

    ReplyDelete
  10. duh! naona hili tatizo liko kwa familia nyingi sana za Africa mimi pia nilipitia hii changa moto mama yangu alikuwa hanipendi kwa sababu sikuwa na kitu na yule mdogo wangu yeye alikuwa na bahati alianza kupata maendeleo mapema kabla yangu so mama akawa anmpenda sana yeye mimi dada mtu nikaonekana choo laki still nampenda sana mama yangu sijali ya nyma namwombea sana kwa Mungu ampe maisha marefu duniani kwa sas maisha yangu sio mabaya Mungu kanisadia atilisti sasa nikisema kitu na mimi nasikilizwa tofauti na before nawaasa wazazi waache kupenda watoto wao kwa ajili ya kuwa na kitu maana wtoto wote ni sawa ukizingatia mmewazaa wenyewe halafu mnakuja kuwachukia kwa vile hawakujaliwa kuwa na kitu na huku hamjui usiku bado mrefu najua hii mada ya leo dada dina aliyoweka hapa itawagusa wengi sana

    ReplyDelete
  11. I like that Dada Dina...u r ryt kabsa.

    ReplyDelete
  12. Dina ubarikiwe saana,nmeanza kukusikia tangu 2006,japo na kama miaka 2 nafatilia kwa kusuasua ila blog yako natembelea nikipata nafasi.natamani kianzishwe kitu kama kipindi cha mzazi na mtoto kwa tv na radio magazeti mitandaoni ili wazazi wajifunze.jamani mzazi ni mwalimu wa kwanza akikosea tu ndo mvurugano kwa akili ya mtoto hutokea.mimi ni msichana na miaka25, kikombe nilichokinywea kimenicost sana hadi inabidi nitumie nguvu.mamangu wa kambo alikuwa ananitukana matusi mzito,mara sura kama pu*bu.mweusi kama giza la m*undu. Ubaguzi,sio siri imeniathiri sana kisaikolojia.maana nilitendewa ukatili wa kutisha.nisaidieni namba za mwanasaikolojia nmweleze maana naweza hata kulipa kisasi.

    ReplyDelete
  13. Duuu imenikumbusha mbali ctaki hata kukumbuka

    ReplyDelete
  14. Wa mama tupunguze ukali was maneno

    ReplyDelete
  15. Sory da dina..hi blog imekufa nini?? Mana hakuna update kbsa,,,,.tunaomba utujulishe ili tuache kuingia... nice time

    ReplyDelete
  16. were are you mama umepotea Dina jaman post kitu kipya!

    ReplyDelete