Wednesday, October 15, 2014

MAISHA BAADA YA KUWA MAMA:JE NI MUDA GANI SAHIHI KUKUTANA KIMAPENZI NA MWENZI WAKO BAADA YA KUJIFUNGUA??

Habari yako da dina,mm naitwa Pendo,nna umri wa miaka 25 nimeolewa na nimebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume wamepishana mwezi mmoja na siku moja na Zion huyu ni wa mwezi march tar 15.Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa kutupatia mwanga wa maisha,inshort kwamba wewe ni kioo changu napenda kuwa kama wewe msikivu, mwerevu, mpenda watu ,muelimishaji rika nk.

Nia na dhumuni la kuandika email hii naomba msaada wako da dina kuna watu wanasema kwamba ukisha jifungua hupaswi kukutana na mumeo kimwili mpaka mtoto atembee la sivyo utambemenda mtoto, wengine wanasema kwamba unafanya ila ukimaliza pale ukaoge kabla hujamshika wala kumnyonyesha mtoto la sivyo utamuharibu atakuwa atembei atakuwa kutwa anafanya kazi ya kuharisha tuu na afya yake itakuwa hafifu kiujumla.Mimi mume wangu ameondoka mda tangu mimba yangu haija pea yupo UK anasoma na amepata kazi huko na mwishoni mwaka huu anarudi kuja kuiona familia yake pamoja na mm mkewe ss hapa ndo najiuliza akija nimwambie tusubiri mpaka mtoto atembee?na je atanielewa kweli? au kuna njia nyingine safe ya kukutana na mumeo bila mtoto kuharibika kiafya?nisaidie dada yangu yamenifika shingoni hata kwa watu niulizie me huwa situmii njia yeyote ya uzazi wa mpango zaidi ya calendar tu ndio safe kwangu.Pls naomba msaada wa mawazo.



*Wapenzi kama mjuavyo na mie ni mama mpya basi tueleimishane.Tunaomba msaada wa kimawazo kulingana na unachofahamu.*

31 comments:

  1. Pole mpenz mie laitwa lamya na tumepishana siku nne kujifungua mie 19 march.kwa uwelewa wangu mdogo mtoto habemendeki kwa kufanya mapenz hapana mie hua nafanya kila anapo nihitaji mumewangu isipokua yeye kawa mstarabu anajua nachoka saana na shuguli za mtoto na kunyonyesha hatufanyi kama zamani na mtoto wangu anaafya namshkurumungu mungu anakilo 10.5 mabibi zetu walikua wajanja saana zamani kulikua hamna uzazi wa mpango na elimu ya uzazi jinsi ya kujikinga na mimba ndio maana wakaogopeshwa kufanya eti wataharibika kama ukiwa na mimba unaambiwa usile mayai mwanao utamzaa kipara sio kweli mpenz usile mayai kwa ajili utazaa mtoto mnene na hapakua na opretion zamani soo nivitu vya kuogopeshana.wewe onana na dactari wako ukiwa na mumeo mupange njia sahihi ya kuzuiya mimba na muenjoy coz akija anahitaji kuenjoy na mkewe safari ni ya mda mpenz uwe makini na mimba ili mtoto akue vizuri.pitia instagram umuone Lamyaseif.

    ReplyDelete
  2. Hi Dina na mtoa mada
    kwa mtazamo wangu. Hakuna mahusiano yoyote kati ya mtoto wako kuathirika kiafya na kufanya mapenzi na mumeo. hizi nni tamaduni tu na mila ambazo hazina ukweli ndani yako. Cha msingi usafi uendelee ukishafanya tendo la ndoa,kwa hali ya kawaida si unajisafisha kabla ya kufanya mambo mengine, mojawapo ni kunawa kabla ya kumshika mtoto. n.k. Hivyo mumewe akirudi toka masomoni endelea na tendo la ndoa kama kawaida. kuna stori nyingi mnoooo utazipata na kuzisikia. kuwa tu mwangalifu, ujue lipi ni kweli na sahihi. mpigie simu gynochologist wowote mwambie hili atakuambia ukweli. Hakuna uhusiano wowote ule kibailojia au kisayansi unacho hakikisha haya uliyosema. mtoto wa miezi tisa sasa hata kama umefanyiwa operesheni umepona kabisa. Mimi nina mtoto wa pili sasa, ana miezi kama sita hivi, nilivyopona tu kama miezi mitatu/miwili baadae nilianza tena kufanya tendo la ndoa.

    ReplyDelete
  3. Hi Dina,
    Me ni mama na nina watoto wa2 na Mimba ya karibia kujifungua, mtoto wangu wa kwanza ana miaka 12 na wa pili ana miaka 6, wote ni wa kiume.
    Kuhusu hilo swali alilouliza mdau kwa upande wangu nakataa sio kweli kwamba ukishirikiana na mmeo mtoto anaharibika, ila ni kwamba endapo utashirikiana na mtu ambaye si baba wa mtoto means mchepuko na ukimnyonyesha mtoto au kumshika mtoto bila kuoga vizuri na kusafisha maziwa basi ujue lazima mtoto ataharibika tuu yani utambemenda mtoto.
    ila kama ni mmeo na ndie baba wa mtoto basi ikishafika miezi mi3 unaruhusiwa kuendelea kudo kama kawaida na mtoto hawezi kuharibika hata kidogo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kumradhi dada, una miaka mingapi sasa? Natamani kuongeza mwana ila wanangu wakubwa Kama wewe, sasa kusoma hapa kuwa unategemea umenipa kimshawisho mwenzangu! Kama hu mind naomba nijue umri wako, wangu ni 42!! Au ndio nshazeeka jama?

      Delete
    2. Hatujazidiana sana, kwa sasa nina 41yrs n 2 month!.. na wala hujachelewa sana kama una nia we beba ndipo upumzike sio uje ubebe ukiwa na miaka 50 na kitu huko!..

      Delete
    3. Nashukuru sana umenipa moyo, kila la kheri na safari yako, Mola akutangulie

      Delete
  4. Haya wajuzi wa mambo haya tiririkeni mtujuze nasi maana tupo wengi

    ReplyDelete
  5. Kitaalamu mama aliyejifungu anaruhusiwa kukutana na mume wake baada ya wiki 6 ni ruhusa Kufanya ten do la ndoa, Kama hana shida na ni mzima kiafya hakuna theory ya kubemenda mtoto katika tendo la ndoa isipokuwa lishe duni ndio inayosa babisha mtoto aonekane kabemedwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio mtaalamu wa masuala haya ila nimesoma makala moja dailymail naona upo sahihi..kuna mama kajifungua mapacha watatu..ila wamepisha miezi saba na kaka yao yaani mama yao alipata mimba yao mwezao akiwa na wiki8...ukisoma hiyo makala hakuna chochote walichoelezea kuhusu wao kufanya mapenzi wakati mtoto ana wiki8 tu....

      Delete
  6. Unaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa baada ya wiki sita, baada ya ile check up ya wiki sita kama huna tatizo. Kama kuna tatizo basi dakatari atakuambia usubiri zaidi. Kwa huku niliko siku unakuwa discharged baada ya kujifungua daktari husema kabisa tena na mume akiwepo "no sex until six weeks ok?!..." Ila kuna wengine huibia na kufanya kabla ya hapo......

    ReplyDelete
  7. Nilijarbu kuulza maana ya kubemenda nkaambiwa kuwa kubemendwa kwa mtoto kunatokea pale unapobeba mimba wakat bado unanyonyesha mtoto mwngne!pale ndyo mtoto anaponyonya maziwa ya mwenzie alye tumbon ndpo anabemendwa mtoto!Na kuhusu muda sahihi inategemea na hali ya mama baada ya kujfungua na ndyo maana kuna cku 40 zle ambazo unatakiwa ukae ndan ili kuchek afya yako na ya mtoto!kama utakuwa poa baada ya cku 40 waweza endelea na mwenza wako kushrk tendo la ndoa!

    ReplyDelete
  8. Jamani muangalie sana! Kuna kipindi cha nyege baada ya kujifungua...

    ReplyDelete
  9. Dina samahani sana. Nitauliza swali off topic kbsa. Nje ya mada kbsa. Najua wewe ni mtu wa jamii. Nitaenda kifupi, nimeguswa na kusaidia watu wenye changamoto ya ulemavu(miguu), sihitaji publicity wala camera nia yangu kusaidia na kuondoka. Nisaidie kuwajua watu wawili tuu. Tutawasaidia baiskeli zile za kutembelea. Asante kwa msaada
    Nicheki 0713297066. Niko serious si utani huu. Sijui pa kuanzia...

    ReplyDelete
  10. Swala la kubemenda halipo kbsaaaa kisayansi hata ukichepuka. Baada ya wiki 6 unaruhusiwa kufanya mapenzi hasa baada ya kumuona dokta

    ReplyDelete
  11. Jamani za kubemenda za zamani Tusiishi karne mia zilizopita wapedwa .Damu ikikatika tuu wewe ruksa.'

    Mimi nimezalia Europe nilipobeba mimba ya kwanza nilibarikiwa kujifungua kwa njia ya operationi kutokana na nyonga zangu kuwa TIGHT. nikarud na kachanga changu na maelekezo narusiwa kufanya SEX damu ikikatika ( Namie nilikuwa na zile miezi 6 ndo nicheze )kikiwa na miezi 3 ikanilazimu niingie shule na nina mshono .nikaenda shule na huku kuna baridi sikuumwa mshono wala nini mwanangu akiwa na miezi saba nikiwa Bongo nikaamua kubeba mimba ili nizae nipumzike . nikazaa.na nilimnyomyesha mpak akaacha.
    Kuna vitu tunavikuza bila sababu eti ukizaa chini kunakuwa pakubwa kakwambia nani .Mungu anamaajabu yake .Kikubwa mjizuie kwani ni rahisi kushika mimba

    Kingine tunakamuaga maziwa tukirudi maziwa hayachachuki wala mtoto haarishi kwa ajili mama alikaa juani.
    Mie nimejaaliwa dodo nilikuwa nakamua maziwa mengi nayafriza nikitoka nabeba yanayayukia njiani ,napasha ktk micro nampa, Cha muhimu usafi.
    ila mkitaka kukamua nunueni japo mashine ya kichina kwani kukamua kwa mikono kunafanya maziwa yanaanguka zaid. Niliambiwa na daktar wa watoto

    ReplyDelete
  12. kitaalam, mzazi ana siku 40 za kitabibu za kupona sawa sawa baada ya kujifungua. wengine wanaziita arobaini ya mzazi/mtoto. Ile ipo kitaalam kabisa. Kwa wanaozaa kawaida ina apply 100%. Sina uhakika na wanaozaa kwa c-section ila nafikiri ni sawa. Hii ni kwa sababu ndani ya siku arobaini uzazi wa mwanamke bado uko wazi na akifanya mapenzi ni rahisi kutunga mimba. Mwanaume anatakiwa aelewe kipindi hiki. suala la nyege aweke pembeni na afikirie kupona kwa mwenzake.

    Pia, after 40 days mwanamke anaweza kutumia any contraceptive...ni salama zaidi sababu ya kupunguza likelihood ya ku conceive mapema. siku hizi mabinti/wamama hawapendi kutumia njia hizi ambapo hufanya wengi kushika mimba mapema wakati mtoto bado anahitaji huduma ya mama. Katika njia nzuri na salama ni condom ofkoz, but mara nyingi wanaume hawapendi condom esp walio katika ndoa, hivyo nashauri njia ya loop. Its safer na husikii chochote wakati wa tendo. Pia haina maudhi kabisa.

    I wish i could write forever, but kwa leo ni hayo tu.

    ReplyDelete
  13. mtoto ataaalibika kama ukifanya mapenzi na mtu ambae sio baba wa mtoto,mchepuko...kama unanyonyesha husifanye mapenzi na mchepuko...NEVERR

    ReplyDelete
  14. mdau hapo juu hakuna isue kama hiyo kumbemenda mtoto ukimnyonyesha wakati uko mjamzito unamnyonyesha vizuri na wala hamdhuru mtoto according to doctors na ukipata mimba kama mtoto wako bado mdogo doc anakwambia endelea kumnyonyesha mtoto ilatu ule vizuri haina madhara kabisa.kwa isue ya kufanya mapenzi as wadau wengine wamesema ni after 6weeks au zaidi kutokana na vile wewe unavyo jiskia mwili wako uko sana .am out yooo.......

    ReplyDelete
  15. Unaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa baada ya wiki sita ya kujifungua tu,kikubwa ni kumtunza tu mwanao na kumlisha vzr hiyo habari ya kubemenda mtt haipo kabisa.Mimi binafsi nna mtt mkubwa tu ana mwaka na miezi mitatu sasa nnashiriki tendo la ndoa na mume wangu na mwanangu ana afya yake nzuri tu,so dada usiogope jiachie na mumeo

    ReplyDelete
  16. Mdau 9:20 si kweli kwamba ukiwahi kubeba mimba unanyonyesha mtoto akanyonya maziwa yako ndo una mbemenda, mimi nina ndugu yangu alimbebea mtoto mimba akiwa mdogo but dr alimshauri huyo dada aendelee kumnyonyesha tu na hakuwa na tatizo lolote tena alikuwa bonge balaa, ujauzito ulipofikisha miezi mitano ndo akamuachisha mtoto wake.
    Hizo ni imani tu hazina ukweli hata chembe!!

    ReplyDelete
  17. Wapendwa nilizaa tarehe 25/9mwaka jana baada ya wiki sita nikaanza ku du na mme wangu mtoto hakudhurika kabisa na sasa kakubwa tu kanene kachangamfuna mwenye afya u nzuri tahadhari jaribu kuonana na daktari wako kupanga uzazi, malezi ya mtoto na mda wako wa kupumnzika inshalaah Mwenyezi Mungu awajalie.

    ReplyDelete
  18. nami nashiriki kwa kusema kuwa hakuna mahusiano ya mapenzi na afya ya mtoto. hivyo ukibahatika kubeba mimba huku unanyonyesha hakuna madhara. na unaruhusiwa kumnyonyesha mtoto mapaka ukiwa na mimba ya miezi saba ndio unaacha kujiandaa kujifungua

    ReplyDelete
  19. Ukimaliza 40 tu kula mzigo

    ReplyDelete
  20. Hi.! Dina
    Mambo Pendo.Okey P kitabibu unaruhusiwa kudu siku40 baada ya kujifungua na kama uko vizuri kiafya na tayari kisaikolojia kuduu kama umejifungua kwa operation huwa wengi wanapenda kusuburi angalau kwa miezi miwili hapo mnaanza kwa mwendo wa pole cku znavyosonga mnaendelea na kasi zenu ukiwa Kati Kati ya kuduuđź’Ź mtoto akahitaji nyonyo jifute jasho kwenye nyonyo mpe atulie muendelee huo ni usafi binafsi kuduu kwa mume na mke hakumuathiri mtoto.Cha muhimu jifeel kuwa uko sexđź’‹ na jiweke kiromantic cz kina mama wengi wanapoteza hamu ya tendo cz anajiona ame gain weight hana mvuto tena jikubali cz ulifanya kazi nzuri ya kumleta kiumbe mzuri duniani gym itafuata tu. đź’•jitahidi kumpa ur hubby nafasi na haki yake jitahid Ku balance kati ya mtoto na baba cz wote wanakuhitaji na wanawivu kwako! Wakati wa kuduu ni dunia yako na mumeo jitahidi iwe hivyo cz utakuwa umeshazoea ukaribu na mtoto..! DEAR ENJOY SEX WIT UR HUBBY. MAPENZI NI SANAA YANAHITAJI UBUNIFU, NIKIPAJI TULICHOZAWADIWA NA MUNGU KITUMIE VIZURI KWA MUMEO NA MUME TUMIA KWA MKEO.Steylapariss

    ReplyDelete
  21. Nilijarbu kuulza maana ya kubemenda nkaambiwa kuwa kubemendwa kwa mtoto kunatokea pale unapobeba mimba wakat bado unanyonyesha mtoto mwngne!pale ndyo mtoto anaponyonya maziwa ya mwenzie alye tumbon ndpo anabemendwa mtoto!Na kuhusu muda sahihi inategemea na hali ya mama baada ya kujfungua na ndyo maana kuna cku 40 zle ambazo unatakiwa ukae ndan ili kuchek afya yako na ya mtoto!kama utakuwa poa baada ya cku 40 waweza endelea na mwenza wako kushrk tendo la ndoa!

    ReplyDelete
  22. hakuna uhusiano wowote hapo ni kumtunza mtoto vzr na kuhakikisha anapata balanced diet.out of topic kwa wanaotaka kupungua nna food supplement ndani ya siku 9 unakua bomba na wanaotaka watoto tuwasiliane 0769119295.

    ReplyDelete
  23. Mi niko na swali kwa wale wanaomkataza asile raha na mume wake kwa madai atam'bemenda mtoto, sasa na wale wadada wako kwenye ndoa mtoto wa pili anabeba mimba ya mwanaume mwengine, after that Mr wa ndoa anaendelea kula mpaka mtoto anazaliwa akijua ni wake na baada ya siku 40 anaendelea kula raha zake, mbona mtoto hapo haonekani kubemendwa??

    ReplyDelete
  24. Unaruhusiwa kufanya tendo la ndoa ukishapona, sema tuu zingatia usafi..after ku duu kaoge vzr. Mm nina watoto 2 wa kwanza nilivyopona tu baada ya wiki 2 nilifanya, wa pili sikushonwa soo aftr six days nilikua powa kabisa nika duu. Na wanangu wana afya nzuri na hawajachelewa kutembea, with one yr wanakua wameanza kutembea. Ww fanya tuu ila uwe makini kama haupo tayari kubeba kwa wakati huu.

    ReplyDelete
  25. Sorry. mi nko na swali lingine tofauti.
    Na mama akiwa mjamzito anashauriwa kushiriki tendo la ndoa na mumewe adi ujauzito ufikishe miezi mingapi kabla ya kujifungua?

    ReplyDelete
  26. kama uko fiti hata baada ya wiki mbili inawezekana ila sio kwa spid kama ile ya zamani

    ReplyDelete